Nani mwalimu wa ndoa by Bahati Bukuku

Image By Mood Converter

lyrics for Nani mwalimu wa ndoa by Bahati Bukuku

Natafuta mshauri popote alipo, oooh. Natafuta mwalimu popote alipo, oooh. ×2

Natafuta mshauri popote alipo, oooh.

Nani Mwalimu wa ndoa, anifundishe na mimi nimuelewe.

Nani mwalimu wa ndoa, aniifundishe nami nijifunze upya. ×2 Ninapo tafuta majibu kwa wengi, Sijapata ni nani wa kujibu swali languuu.

Ninapo fanya utafiti kwa wengi, sijapata mtu wa kujibu swali languuu.

Nani, mwaalimu mzurii, nani, mshauri mzurii. Darasa la kwanza, mpaka la saba nilipo maliza walinipa cheti. Sekondari na vyuo vyote, mwisho wa masomo walinipa cheti.

Lakini, kitu ndoa. Nilipoonyesha moyo wa kujiunga na hii taasisi, sijui shirika.

Kabula sijafuzu masomo walimu wangu walinipa cheti.

Nilipoonyesha nia ya moyo walimu walinipa cheti.

Kinachonitia uchungu zaidi, Walimu waliofundisha vyema.

Kesho unamkuta darasani tena, anageuka kuwa mwanafunzi upya.

Na yule aliyefundishwa jana, anageuka kuwa mwalimu. Oooh-ooooh.

Hakuna kitu kibaya kama ndoa ikikosa Amani, hata ukicheka unaonekana unazomea.

Hakuna kitu kibaya kama ndoa ikipoteza upendo, Hata ukipata mafuta unaonekana umepakaa vumbi eeeh. Nani mwalimu wa ndoa, anifundishe na mimi nimuelewe.

Nani mwalimu wa ndoa, anifundishe nami nijifunze upya.

Nani mwalimu wa ndoa, anifundishe na mimi nimuelewe.

Huwezi kutumia kanuni ya ndoa yako, Ili itumike kutibia ndoa ya mwingine.

Huwezi kutumia kanuni ya mtu mwingine, Ili uweze kuponya ndoa ya kwako weeeh.

Huwezi kutumia tabia ya mume wako, Ili uweze kurekebisha mume wa mwingine.

Huwezi kutumia mke wako, ili uweze kurekebisha mke wa mwingine.

Nani mwalimu wa ndoa, anifundishe na mimi nimuelewe.

Nani mwalimu wa ndoa, anifundishe nami nijifunze upya.

Neema ya mungu inahitajika hapo, neema ya mungu, (kwa mume wako).

Neema ya mungu inahitajika hapo, huruma ya mungu (kwa mke wako).

Neno la mungu linahitajika, neno la mungu (omba kwa bidii)×2.

lyrics by claudine

Leave a Reply

Your email address will not be published.